🎶 BARAGUMU ITALIA SANA, Louange TABERNACLE CHRÉTIEN DE LUBUMBASHI

0 Görünümler
admin
admin
11/08/26

🎶 BARAGUMU ITALIA SANA, Louange TABERNACLE CHRÉTIEN DE LUBUMBASHI

1Baragumu litalia sana, watu wote watalisikia. Waliokufa watafufuka na wazima watabadilika.
:/: Nani anayeweza? Yesu, mweza yote.:/:

2Na wenye uwezo wa dunia watatetemeka siku ile, na hawataweza kuinuka kutazama uso kama jua.
:/: Nani anayeweza? Yesu, mweza yote.:/:

3Najua Mchunga wangu mwema, anichunga kwa maisha yangu. Na siku ya mwisho nikishinda, sitaona uchungu wa kufa.
:/:Nani Mchunga mwema? Yesu, mweza yote.:/:

4Mbinguni hakitafika kitu cha uchafu, dhambi na kuasi. Wasiomwamini Bwana Yesu, gadhabu ya Mungu yawangoja.
:/: Nani atahukumu? Yesu, mweza yote.:/:

5Mimi Yesu mzabibu kweli, Baba Mungu ndiye mkulima, na ninyi matawi ndani yangu, na hamwezi neno bila mimi.
:/: Nani ni mzabibu? Yesu, mweza yote.:/:

6Unayempenda Baba Mungu, lazima upende ndugu yako; ukiwa hupendi ndugu yako, huwezi kupenda Baba Mungu.
:/:Nani aliyesema? Yesu, mweza yote.:/:

7Nawapenda, mwisho wa upendo, na ninyi mpate kupendana; hivyo mataifa wataona ya kwamba m watu wangu kweli.
:/: Nani mwenye upendo? Yesu, mweza yote.:/:

8Sisi watumishi wake Mungu, tumeacha vyote vya dunia. Tumemchagua Bwana Yesu, tuwekwe kuume kwake Mungu.
:/: Tumshukuru nani? Yesu mweza yote.:/:


#tabernaclechretiendelubumbashi #cantique #louange #nyimbozawokovu #nyimbozamungu

Daha fazla göster

0 Yorumlar Göre sırala

Hiçbir yorum bulunamadı

Bir sonraki