DAMU YAKO YENYE BARAKA — NYIMBO ZA WOKOVU N°10 | Swahili Worship Hymns

0 Lượt xem
admin
admin
11/08/26

DAMU yako yenye baraka
Inayotuosha makosa,
Ilimwagwa msalabani,
Bwana Yesu, ulipokufa.
Nastahili 'pata hukumu,
Na siwezi mimi kujiosha.
Unioshe katika damu
Nipate kuwa safi kabisa!

Safi, safi kweli,
Safi, safi kweli!
Unioshe katika damu,
Nipate kuwa safi kabisa!

Yesu, ulivikwa miiba,
Kuangikwa juu ya mti
Ulivumilia mateso,
Maumivu na majeraha.
Ninataka kijito hicho,
N’ende na nikasafishwe sana!
Unioshe katika damu,
Nipate kuwa safi kabisa.

Safi, safi kweli,
Safi, safi kweli!
Unioshe katika damu,
Nipate kuwa safi kabisa!

Baba, kweli nina makosa,
Moyo wangu wa udhaifu;
Mimi mwenye dhambi rohoni
Nitaona wapi Mwokozi ?
Yesu, kwako msalabani
Naja, Ninakuamini sasa.
Unioshe katika damu,
Nipate kuwa safi kabisa.

Safi, safi kweli,
Safi, safi kweli!
Unioshe katika damu,
Nipate kuwa safi kabisa!

Bwana, nimefika karibu,
Unilinde kwako milelee!
Ufungue kila kikamba,
Unijaze moyo mwenyewe.
Nakaribu ya msalaba
Nitakaa hata kufa kwangu.
Unioshe katika damu,
Nipate kuwa safi kabisa!

Safi, safi kweli,
Safi, safi kweli!
Unioshe katika damu,
Nipate kuwa safi kabisa!

Cho xem nhiều hơn

0 Bình luận Sắp xếp theo

Không có bình luận nào được tìm thấy

Tiếp theo