MAISHA MAFUPI - NYIMBO ZA WOKOVU no 79
0 Visningar
admin
11/08/26
1. Maisha yamafupi
ya hapa dunia
yanaifanana safari chomboni.
Twapita bahari katika hatari,
lakini Mwokozi anatuongoza.
Ikiwa Mwokozi anatuongoza
twaweza kuona amani na raha,
atatufikisha salama mbinguni,
na humo hatutakumbuka safari.
2. Twapita katika baridi na pepo,
maneno ya Mungu ni nuri gizani.
Hatari na hofu na chombo kibaya hatuta’kumbuka karibu na Yesu.
3.Ingawa mawimbi yapiga kwa nguvu, tunakaribia bandari upesi.
Na humo hakuna dhoruba na pepo;
safari tutaimaliza salama.
4. Tutakapofika bandari ya mbingu tutamshukuru Mwokozi mkuu.
Hatutaziona hatari na hofu
karibu na Yesu mwenyewe mbinguni.
-
Kategori
Visa mer

Inga kommentarer hittades