Mimi mwenye hatia 291 Nyimbo za wokovu

0 Visningar
admin
admin
11/08/26

291 Nyimbo za wokovu
Mimi mwenye hatia
nilikombolewa, Mwokozi
alipojitoa. Dhambi zangu na
zako alizichukua,
kwa damu aliniokoa.
Ref:
Dhambi zimetundikwa
msalabani alipojitoa, Mwokozi.
Alidharauliwa na kukataliwa
atupatanishe na Mungu.

2
Yesu mwenye upole
na mwenye upendo
ananitakasa rohoni.
Nimepata uhuru
kwa Yesu Mwokozi,
alikufa msalabani.

3. Namwambata Mwokozi, sitaki
kumwacha, kwa kuwa alinifilia.
Nakusifu, e’ Yesu, unayenipenda,
daima nakushangilia.


#Nyimbozawokovu

Visa mer

0 Kommentarer Sortera efter

Inga kommentarer hittades

Strax