MWOKOZI WETU ANATUPA FURAHA DUNIANI — Swahili Worship Hymns — NYIMBO ZA WOKOVU 141
MWOKOZI wetu anatupa
Furaha duniani,
Atuongoza kwa neema
Na anatushibisha.
Tazama Yupo pamoja nasi,
Neema haitaisha kamwe!
Haleluya, Haleluya,
Haleluya, Amina!
Ni vema kumpenda Mungu
Aliyetukomboa,
Vizuri kuwa mtu wake,
Sitapotea kamwe.
Furaha yetu itabakia,
Ikiwa vyote vingetoweka.
Haleluya, Haleluya,
Haleluya, Amina!
Ikiwa giza mara nyingi,
Na jua likifichwa,
Na tukijaribiwa huku,
Twajuwa ni kwa muda.
Mbinguni hatutaona kamwe
Huzuni wala machozi tena.
Haleluya, Haleluya,
Haleluya, Amina!
Na tusisumbukie tena
Chakula wala nyumba,
Maana vyote twavipata
Kwa neema yake Mungu.
Njiani yote atuongoza,
Aichukuwa mizigo yetu.
Haleluya, Haleluya,
Haleluya, Amina!
Ikiwa vema huku chini
Kutegemea Yesu,
Furaha gani huko juu
Kuona uso wake!
Tutaiona furaha tele,
Na utukufu hautaisha,
Haleluya, Haleluya,
Haleluya, Amina!
-
categoría

No se encontraron comentarios