Nataka kupokea baraka yake Mungu 150 NW

0 مناظر
admin
admin
11/08/26

150 NATAKA kupokea baraka yake Mungu

Nyimbo Za Wokovu 

1. Nataka kupokea baraka yake Mungu,
nataka kubatizwa kwa Roho ‘takatifu.
Ju’ ya ahadi yake napumzika sana,
aliahidi mimi kupata Roho yake.

Pambio:
Sawa na bahari, sawa na bahari
ni neema yake anileteayo. Anayenijaliza,
anayeniponyesha, ni Mwokozi wangu.
Asifiwe sana!
 

2. Kanisa lake Mungu linaipata mvua,
vijito vya baraka vinamiminwa sasa.
Furaha ya uzima ni kubwa kati yetu.
Tuimbe haleluya! Tumshukuru Yesu!
 
3. Mawimbi ya wokovu yanatujia sasa.
E’ Mungu, tunaomba: Ujaze sisi sote!
Watakatifu wako watakasike sana!
Tuimbe haleluya! Tumshukuru Yesu!
 

4. Mawimbi ya wokovu yaliyofika kwetu,
E’ Mungu, uyatume ulimwenguni mwote,
maelfu kati watu wapate kuokoka,
waimbe haleluya, wamshukuru Yesu!

#Nyimbozawokovu

مزید دکھائیں

کوئی تبصرہ نہیں ملا

اگلا