Niliye Msafiri – Nyimbo za Wokovu 75
[Verse 1]
Niliye msafiri, mgeni duniani;
Sioni kwangu hapa, ni huko ju’ mbinguni.
Ninatamani nami kukaa siku zote
Pamoja naye Baba Katika utukufu.
[Refrain]
Kwangu mbinguni, kwangu,
Kwangu mbinguni, kwangu,
uzuri wa mbinguni wapita yote huku.
[Verse 2]
Mwokozi Yuko huko, Rafiki yangu mwema,
Aliyenikomboa na ku’chukua dhambi.
Na hata nikiona furaha siku zote
Ningalinatamani makao ya mbinguni.
[Verse 3]
Na nikipewa huku vipawa vya thamani,
Na wakiimba nyimbo za kunifurahisha,
Rafiki wangu wote wakipendeza mimi,
Ningali natamani makao ya mbinguni.
[Verse 4]
Upesi nitaona kifiko cha mbinguni,
Mwokozi wangu Yesu atanikaribisha;
Na huko nitaona nilivyotumaini,
Kinubi nita’piga kumshukuru Yesu.
#nyimbozawokovu #NiliyeMsafiri #HymneSwahili #adoration #musiquechrétienne #NyimboZaKiroho #wokovu #rdc #tanzania #kenya #ouganda #burundi
-
Kategorya

Walang nakitang komento