NINAKUMBUKA sayuni ( 84 NW )

0 ভিউ
admin
admin
11/08/26

84 NINAKUMBUKA sayuni

Nyimbo Za Wokovu
#Nyimbozawokovu

1. Ninakumbuka Sayuni, nchi ya heri
mbinguni, bahari kama kioo
na’furahia rohoni. Nyuma kimeta cha nuru
Naona mji wa mbingu,
nyimbo za nyumba ya Baba
nasikiliza daima.

Pambio:
Mapambazuko mbinguni
yataondoa utaji,
vyote tulivyoamini
tutaviona milele.

 
2. Mauti haina nguvu, Yesu a’vunja uchungu,
naye aliwakomboa wote; wafalme,watumwa.
Ninamtwika Mwokozi dhambi, huzuni na shida;
mbavuni mwake nafasi kama bandari salama.
 
3. Kuna ‘jaribu njiani, mengi yakunizuia,
na mara nyingi miiba, inaumiza miguu.
Nikikumbuka Sayuni moyo huwaka kabisa,
mbingu ninaitazama na ku’himiza safari.

আরো দেখুন

0 মন্তব্য ক্রমানুসার

কোন মন্তব্য পাওয়া যায়নি