Pata Faraja na Amani: Jina Lake Yesu Tamu | Tenzi za Rohoni

0 ভিউ
admin
admin
11/08/26

Karibu kusikiliza JINA LAKE YESU TAMU – Tenzi za Rohoni No. 5, wimbo wa baraka, ibada na kumtukuza Bwana Yesu Kristo. Wimbo huu wa injili ya Kiswahili unaleta faraja, tumaini na nguvu za kiroho kwa kila msikilizaji.

Ikiwa unapenda nyimbo za injili za Kiswahili, tenzi za rohoni, nyimbo za wokovu na nyimbo za kuabudu, usisahau:

✅ Subscribe
✅ Like
✅ Comment
✅ Share

Mungu akubariki kwa kutazama na kuunga mkono huduma ya Swahili Gospel Sounds.

#JinaLakeYesuTamu #TenziZaRohoni #SwahiliGospel #NyimboZaWokovu #GospelMusic #YesuKristo #ChristianMusic #SwahiliGospelSounds

Jina lake Yesu tamu;
Tukilisikia
Hutupoza, tena hamu
Hutuondolea.

Roho iliyoumia
Kwalo hutibika,
Chakula, njaani pia;
Raha, tukichoka.

Jina hili ni msingi,
Ngao, ngome, mwamba,
Kwa hili napata wingi,
Kwangu ni akiba.

Yesu, Mchunga, Rafiki
Mwalimu, Kuhani,
Mwanzo, Mwisho, Njia, Haki,
Uzima kifoni.

Moyo wangu hauwezi,
Kukusifu kweli,
Ila sifa zangu hizi,
Bwana zikubali.

Na utakaponiita,
Kuja kwako Bwana,
Huko kwako sitaacha
Kukusifu sana.

আরো দেখুন

0 মন্তব্য ক্রমানুসার

কোন মন্তব্য পাওয়া যায়নি

পরবর্তী আসছে