SITASUMBUKA — Swahili Worship Hymns — NYIMBO ZA WOKOVU 50

0 vistas
admin
admin
11/08/26

Sitasumbuka kwa kuwa Mungu
Ananitunza daima,
Anachukuwa mizigo yangu
Nyakati zote za mwendo.

Sijaiona nyingine siku,
Na jana imetoweka,
Na leo Mungu anazijuwa
Hitaji zote ninazo.

Sitasumbuka kwa kuwa Mungu
Ni baba yangu kabisa.
Hawezi kunisahau mimi
Ingawa akijificha.

Sijaiona nyingine siku,
Na jana imetoweka,
Na leo Mungu anazijuwa
Hitaji zote ninazo.

Sitasumbuka kwa kuwa Mungu
Anishibisha néema,
Anipa yote yanifaayo
Kwa roho yangu na mwili.

Sijaiona nyingine siku,
Na jana imetoweka,
Na leo Mungu anazijuwa
Hitaji zote ninazo.

Mauwa yote anayavika,
Na ndege wote wa anga
wanapokea chakula chao
pasipo shamba na ghala.

Sijaiona nyingine siku,
Na jana imetoweka,
Na leo Mungu anazijuwa
Hitaji zote ninazo.

Ninafurahi katika Bwana,
Na kama ndege naimba.
Najuwa kwamba nyakati zote
Babangu ananitunza.

Sijaiona nyingine siku,
Na jana imetoweka,
Na leo Mungu anazijuwa
Hitaji zote ninazo.

Mostrar más

0 Comentarios Ordenar por

No se encontraron comentarios

Hasta la próxima