Ufurahi moyo wangu 133 Nyimbo za wokovu
0 Vues
admin
11/08/26
UFURAHI MOYO WANGU
133 NYIMBO ZA WOKOVU
1. Ufurahi, moyo wangu,
heri nyingi umepata!
:/: Sikitiko limekwisha,
Yesu ni wangu nami wake. :/:
2. Ameponya roho yangu,
yeye ni mponyaji mwema;
:/: Na kwa Roho ‘takatifu
anabatiza watu wake. :/:
3.Jina langu ni mbinguni,
Yesu ameliandika.
:/: Mimi mali ya Mwokozi
hata milele na milele.:/:
4.Na moyoni mwangu
sasa ninaimba: Mungu, Baba!
:/:Ni furaha kubwa sana,
nina rafiki kila saa. :/:
5.Nimeondolewa dhambi,
nisitende ovu tena!
:/: Kwani Yesu aokoa
kila wakati na dakita. :/:
6.Nyimbo za kusifu Mungu
zinajaa mbingu zote.
:/: Moyo wangu unajibu:
Amina. Mungu asifiwe» :/:
#Nyimbozawokovu
-
Catégorie
Montre plus

Aucun commentaire trouvé