Uzima Ninao Moyoni Daima - Tabernacle Chrétien de Lubumbashi ( Chanson en Swahili )
Uzima Ninao Moyoni Daima - Tabernacle Chrétien de Lubumbashi - Nyimbo za Wokovu 149
1.
Uzima ninao moyoni daima,
Uzima ni Yesu Mwokozi,
Aliyeingia rohoni hakika,
Akanitilia ’hodari.
Chorus
Nashiba rohoni kwa raha ya Mungu,
Na moto wa mbingu ulimo.
Napata kukaa nuruni kabisa,
Na nuru ni Yesu Mwokozi.
2.
Baraka zilizo katika wokovu
Nilizozipata kwa bure,
Nilipoungama makosa na dhambi
Kwa Yesu Mwokozi wa wote.
3.
Mwokozi aliniondoa porini;
Natunzwa shambani mwa Mungu.
Na sasa kwa mvua na jua la mbingu
Ninamzalia matunda.
4.
Naona maisha ni yenye maana:
Ni ku’tumikia Mwokozi.
Kuishi ni Kristo na kufa faida
Kwa kila mkristo wa kweli.
Below is the link to the video where the songs were extracted:
https://www.youtube.com/watch?v=0TA89nt0bqU
Uzima Ninao Moyoni Daima - Tabernacle Chrétien de Lubumbashi ( Chanson en Swahili )
#Maranatha
-
Kategori

Tidak ada komentar yang ditemukan