Yesu Ni Furaha Yangu - Nyimbo za Wokovu 121

0 Visningar
admin
admin
11/08/26

Yesu Ni Furaha Yangu - Nyimbo za Wokovu 121

1.
Yesu ni furaha yangu, Amejaa pendo kweli.
[ Anaweza kusimika Kila mwenye udhaifu. ] BIS
[ Ananipa ujasiri, Nguvu, raha na faraja. ] BIS
[ Hata nikionja kufa, Yesu ni Mchunga wangu. ] BIS

2.
Nimefungwa na Mwokozi Kwa kifungu cha upendo,
[ Hata kufa hakuwezi Kunitenga naye Yesu. ] BIS
[ Mimi wake siku zote, Ninataka kumtii. ] BIS
[ Kwa neema nimepona, Nisitumikie dhambi. ] BIS

3.
Kwa mikono ya upendo Ninakumbatiwa naye,
[ Sitaweza kutafsiri Pendo lake kubwa kwangu. ] BIS
[ Napokea nguvu yake, Yanijaza moyo wangu. ] BIS
[ Yesu ananiongoza Katika safari yangu. ] BIS

Yesu Ni Furaha Yangu - Nyimbo za Wokovu 121

#Maranatha

Visa mer

0 Kommentarer Sortera efter

Inga kommentarer hittades

Strax