YO YOTE uonayo huku katika mwendo wako(16 NW)

0 Lượt xem
admin
admin
11/08/26

16 YO YOTE uonayo huku katika mwendo wako

Nyimbo Za Wokovu 
#Nyimbozawokovu

1. YO yote uonayo huku
katika mwendo wako,
Yafaa kumwambiya Yesu
atakusaidia.

Refrain:
:/: Kwa kuwa kila aombaye
Mwokozi ne’ma yake,
ataokoka na hatia,
na atasifu Yesu. :/:

2. Ukichukiwa na wenzake
na ukijaribiwa,
Mwokozi yu karibu sana,
Maombi asikia.
3. Ukiwa mwana mpotevu,
na mbali na Babako,
Amani una’kosa sasa,
Urudi kwake Yesu!
4. Ukiwa na makosa mengi,
Na roho yako ngumu,
Neema yake yakutosha,
utubu dhambi zako

5. Ikiwa nguvu mara nyingi
kuomba kwa bidii,
uombe Baba, kama mwana,
akusikia kweli!

Cho xem nhiều hơn

0 Bình luận Sắp xếp theo

Không có bình luận nào được tìm thấy

Tiếp theo